
JESHI
la Polisi Mkoa wa Ilala jijini Dar es Salaam linamsaka kwa udi na
uvumba Emmanuel Mbasha (pichani) ambaye ni mume wa mwimbaji maarufu wa
nyimbo za Injili nchini, Flora Mbasha kwa madai ya kumbaka shemeji yake
mwenye miaka 17 (jina tunalo) ambaye ni yatima.

Flora
Mbasha akiwa na mumewe Emmanuel Mbasha anayetuhumiwa kwa ubakaji.
Taarifa zilizopatikana ndani ya jeshi hilo kupitia vyanzo vyetu makini
zinadai kwamba mlalamikaji huyo alifika kituoni hapo Jumatatu iliyopita
muda wa mchana na kufungua kesi yenye Kumbukumbu Na. TBT/RB/3191/2014 na
ya Jalada la Uchunguzi Na. TBT/IR/1865/2014 akidai kufanyiwa unyama huo
kwa siku mbili (Ijumaa na Jumapili) wiki iliyopita nyumbani kwa Mbasha,
Tabata-Kimanga, Dar.
Ilidaiwa kuwa, Ijumaa iliyopita
mlalamikiwa alifanya kitendo hicho sebuleni nyumbani na Jumapili
ilidaiwa alitekeleza ukatili wake huo ndani ya gari lake hali ambayo
ilimfanya mlalamikaji kutoa taarifa Kituo cha Polisi, Tabara-Aroma
jijini Dar.

Mume
wa mwimbaji maarufu wa nyimbo za Injili nchini, Flora Mbasha, Emmanuel
Mbasha anayetafutwa na polisi kwa kosa la ubakaji. Iliendelea kudaiwa
kuwa, kufuatia maumivu makali aliyoyapata mlalamikaji huyo ilibidi aende
Hospitali ya Amana na kugundulika kuwa aliingiliwa kimapenzi na
kumsababishia michubuko sehemu za siri.
HISTORIA YA MLALAMIKAJI
Mlalamikaji ni kati ya watoto mapacha waliozaliwa jijini Mwanza na mama ambaye jina lake halikupatikana mara moja.
Mama wa mtoto huyo (kwa sasa ni marehemu pamoja na mume wake) akiwa
muumini wa Kanisa la Evangelical Assemblies of God (EAGT) aliamua kumtoa
mtoto mmoja kwa mama mzazi wa Flora Mbasha kwa lengo la kumlea, wakati
huo mtoto huyo alikuwa na miezi mitatu.

Flora Mbasha akiwa na mumewe Emmanuel Mbasha.
Ikaelezwa kuwa, mama wa Flora alikaa na mtoto huyo akimsomesha hadi
alipofika darasa la saba ambapo alimkabidhi kwa Flora na kuishi naye
hadi alipofikwa na janga hilo.
Maelezo zaidi yanasema Mbasha aliweza
kufanya kitendo hicho kwa sababu mkewe (Flora) ameondoka nyumbani na
kwenda kuishi hotelini kwa kile kilichodaiwa kwamba kuna ugomvi mkubwa
ndani ya ndoa yao.
Taarifa zaidi zinadai kwa sasa Mbasha naye hayupo
nyumbani kwake huku mlalamikaji yuko Hospitali ya Amana akiendelea
kufanyiwa uchunguzi wa kiafya ili kubaini kama ana maambukizi ya
magonjwa ya zinaa au la!

Wanandoa
hao katika pozi. Kwa upande wake mlalamikaji huyo alipopigiwa simu juzi
kwa lengo la kuthibitisha kuhusiana na sakata hilo alikiri na kusema
amekwishatoa taarifa polisi kwa kitendo alichofanyiwa na mwenye nyumba
huyo huyo. Endelea kusoma Magazeti Pendwa ya Global Publishers ili
kupata mwendelezo wa tukio
hilo.
0 comments:
Chapisha Maoni